Tanzania Breweries Limited
Tanzania Breweries Ltd.
50 Years of Uhuru

KAMPENI ZA MIAKA 50 YA UHURU

Mwaka huu, tarehe 9 Desemba, Tanzania itakuwa inatimiza miaka 50 tangu kupata uhuru. Kilimanjaro Premium Lager, kupitia kampeni yake ya "Jivunie Utanzania" itakuwa ikiwaleta Watanzania pamoja na kuwasherehesha huku ikiwakumbusha kuangalia tunakokwenda bila kusahau tulikotoka.

 

Muhimu zaidi, Kilimanjaro Premium Lager inatuhamasisha kama Taifa tuendelee kufanya bidii ili kupata mafanikio zaidi.


Hivyo basi mimi, wewe na yule tuungane pamoja kujivunia Utanzania wetu na kufurahia bia tuipendayo ya Kilimanjaro Premium Lager, Bonge la Kiburudisho kwa Watanzania.

 

Watanzania tuna mengi ya kujivunia

 

Amani

Tunajivunia amani iliyojengeka na kudumu katika nchi yetu mpaka sasa

 

Kiswahili

Tunajivunia Kiswahili, lugha inayotuunganisha kitaifa.

 

Heshima na Ukarimu

Tunajivunia heshima na ukarimu wetu tulivyorithi kutoka katika mila na desturi zetu.

 

Rasilimali

Kati ya maajabu saba ya dunia, matatu yanapatikana Tanzania ambayo ni hifadhi ya Ngorongoro, bonde la Olduvai na mlima Kilimanjaro. Tunajivunia uoto wa asili, milima yetu, madini yaliyosheheni katika ardhi yetu. Tunajivunia Twiga, mnyama wetu wa Taifa na mbuga kubwa za wanyama.

 

Watu

Tunajivunia waasisi wetu ambao wamechangia kufikia mafanikio tuliyo nayo hivi leo na tutawaenzi wale wanaoendelea kutupeleka mbele kama Taifa.

 

Na tuna mengi zaidi ya kujivunia

Tukiwa tunafikisha miaka hamsini ya uhuru wetu, ni wakati wa kuungana kama Taifa na kukumbuka yale mazuri yanayotuletea sifa na yanayotufanya tujivunie uzalendo.

 

BONGE LA KIBURUDISHO KWA WATANZANIA

Kilimanjaro Premium Lager ni bia ya kujivunia ya Kitanzania inayopendwa na Watanzania wengi ambayo imepewa jina la kuuenzi mlima Kilimanjaro. Ni bia laini yenye kilevi cha wastani, asilimia 4.5, ambayo inatuleta pamoja wakati wote na kutuburudisha na kutufanya tujisikie vizuri kila tunapokunywa.

 

Kilimanjaro Premium Lager ni mahsusi kwa Watanzania ambao wanajivunia asili na utamaduni wao. Kilimanjaro Premium Lager ni bia pekee inayowapa ari na hamasa Watanzania kufikia kilele cha mafanikio kwa yale wanayoyafanya.

 

Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikidhamini michezo na matukio mbalimbali muhimu katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na tuzo za muziki za Tanzania (Kili Tanzania Music Awards), Mbio za Kili Marathon na udhamini wa klabu kongwe za mpira wa miguu: Simba na Yanga.


Miaka 50 ya Uhuru
Radio Advert

UHURU TV AD »

Click here
Follow Kili on YouTube